Subscribe:

Ads 468x60px

Tuesday, 24 July 2012

ZITTO AREJESHA PENZ LA WEMA NA DIAMOND

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, ametajwa kuwa kichocheo cha kurejea kwa penzi la vijana wenye umaarufu mkubwa nchini kwa sasa, Nasibu Abdu Juma ‘Diamond’ na Wema Isaac Sepetu.

Uwazi, lina mkanda wa video, unaowaonesha Diamond na Wema pamoja kwa mara ya kwanza, baada ya muda mrefu wa kutupiana maneno mengi ya kashfa, huku kila upande ukimshusha hadhi mwenzake.
Diamond na Wema, walinaswa kwenye Tamasha la Kigoma All Stars, lililoandaliwa na Zitto kisha kufanyika Julai 17, mwaka huu kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.
Shukurani kwa Zitto, kwani kupitia tamasha hilo, Diamond na Wema, waliweza kudhihirisha kwa kila mtu kwamba uhusiano wao sasa umerejea upya kwa kuambatana kimahaba ndani ya Mkoa wa Kigoma.
SAFARI ILIVYOKUWA TAMU
Watu wengi wakijua kwamba kuna uhasama mkubwa kati ya Wema na Diamond, Julai 17, mwaka huu, ilikuwa ni mshangao wa aina yake kwa waliokuwepo Uwanja wa Ndege wa Mkoa wa Kigoma, baada ya vijana hao kushuka wakiwa wameongozana.

Diamond akiwa amevaa shati jekundu na tai nyeusi, chini akiondokea suruali ya jeans rangi ya bluu iliyopaushwa kimodo, huku Wema akitokelezea kwa koti la rangi ya maziwa, ndani blauzi nyeusi, halafu wote wameyaficha macho yao kwa miwani nyeusi, waliwaka vilivyo ndani ya Ujiji, Kigoma.
Baada ya kuwasili Kigoma, Wema na Diamond walielekea Hoteli ya Tanganyika Beach (ipo ufukweni mwa Ziwa Tanganyika) ambako walipata pumziko walilohitaji kabla ya nyota huyo wa wimbo wa Mbagala, hajaelekea Uwanja wa Lake Tanganyika kwenye Tamasha la Kigoma All Stars a.k.a Leka Dutigite.
WEMA ALIFUATA NINI KIGOMA?
Minong’ono ilitawala kila kona ya Mkoa wa Kigoma kwamba Wema amekwenda kuwakilisha Leka Dutigite, hivyo wakataraji kumuona Uwanja wa Lake Tanganyika, akitoa sapoti yake kwenye tamasha hilo.
Wapo ambao waliacha shughuli zao kwa ajili ya kwenda kumuona Wema tu uwanjani lakini waliambulia patupu, kwani mrembo huyo hakuonekana kabisa.
Kutokana na hali hiyo, wale waliovumisha stori kwamba Wema amekwenda Kigoma a.k.a Lwama, walionekana wazushi wasiofaa kusikilizwa, bila kujua kwamba mtoto alijificha ndani ya Hoteli ya Lake Tanganyika Beach.
HAKIKA WANAPENDANA
Kama ukaribu wao ulisababishwa na tamasha lililoandaliwa na Zitto peke yake, basi wangekuwa na muonekano ‘feki’ sehemu chache wanazopita lakini kinyume chake wao walithibitisha wanapendana haswaa!

Diamond, alishindwa kujichanganya na wasanii wenzake aliokuwa nao kwenye shoo ya Kigoma kama akina Said Juma ‘Chegge’, Peter Msechu, Banana Zorro, Mwasiti Almasi na wengineo, badala yake muda mwingi aliutumia kuwa umbali wa mita sifuri kutoka alipo Wema.
‘Mtundu’ wa nyimbo mbili mpaka sasa, Nai Nai na Baadaye, Omar Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, ndiye pekee aliyekuwa jirani na vijana hao maarufu, walioamua kurejesha penzi lao kupitia mwavuli wa shoo hiyo.

Kwa upande mwingine, ni kama vile waliamua kwenda kufanya tambiko nyumbani asili kwa mume mtarajiwa, yaani Diamond kwa sababu chimbuko la Wema ni Mkoa wa Tabora, japo baba yake, Balozi Isaac Abraham Sepetu, amejichimbia Zanzibar kwa miaka mingi.
Mtu mmoja, mwenye hulka ya kutopitwa na mambo, akamueleza ripota wetu kuwa Julai 18, wasanii hao walikwenda Hifadhi za Gombe na Mahale, mkoani humo lakini jioni yake, Diamond aliongozana na Wema mpaka kwa babu yake, eneo la Ujiji Posta, mkoani humo ambako walisomewa dua na Babu Nasibu.
RAHA NDANI YA TILAPIA HOTEL
Safari ya furaha kwa Wema na Diamond, ilihamia ndani ya Jiji la Miamba ya Mawe, Mwanza ‘Rocky City’ kwenye Hoteli ya Tilapia, iliyopo ufukweni mwa Ziwa Victoria, eneo la Capri Point, hiyo ikiwa Julai 19, 2012.

Habari zinapasha kuwa wawili hao, walipumzika kwenye hoteli hiyo kwa muda mfupi, wakati wanasubiri saa ya ndege yao ya kuwatoa Mwanza hadi Dar es Salaam ifike.

Ndege waliyopanda Diamond na Wema kutoka Kigoma, ilitua Mwanza saa 9:30 alasiri, hivyo kuanzia muda huo, waliutumia Tilapia Hotel mpaka saa 2:30 usiku, wakaripoti Uwanja wa Ndege wa Jiji la Miamba ya Mawe, kabla ya saa 3:50 usiku, usafiri huo wa anga, uliitupa mkono ardhi ya Mwanza mpaka Dar es Salaam.
AIR PORT DAR ES SALAAM
Mama mzazi wa Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra Sammi’, alionekana Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, kuanzia saa 4:45 usiku (Julai 19), hivyo kwa jicho la ripota wetu, ikawa wazi kwamba amekwenda hapo kumpokea mwanaye kipenzi, Diamond ‘Sukari ya Warembo’.

Kutokana na safari hiyo kuwa mguu wa Diamond uliambatana na wa Wema, kwenda kwenye shoo ya kutoa shukurani nyumbani kwao Kigoma, ni wazi Mama Nasibu (Mama Diamond) alikuwa pale pia kwa minajili ya kumlaki mkwe a.k.a Mka Mwana.
PW 415 YAWASILI DAR
Diamond na Wema, walipanda ndege ya Kampuni ya Precision Air, PW415 na ilipotimia saa 5:30 usiku, ilitangazwa kuwa ndiyo inawasili kwenye uwanja huo wa ndege wenye jina la muasisi wa taifa huru la Tanganyika na baadaye Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ‘Baba wa Taifa’.
Milango ya saa 5:52, Diamond na Wema, walipita kwenye mlango wa wanaowasili (arrivals gate), wakiwa sambamba na Ommy Dimpoz, walipokelewa na Mama Nasibu hadi sehemu ya maegesho ya magari uwanjani hapo.

Timu nzima, ilijipakia kwenye gari la Diamond aina Toyota Land Cruiser Prado, rangi ya fedha, wakatoweka eneo la uwanja huo.
DIAMOND KWA WASIWASI
Saa 6:14 usiku (Julai 20), Diamond alimpigia simu ripota wetu, eti akahoji kilichompeleka uwanja wa ndege. Mahojiano yalikuwa hivi;
DIAMOND: Kiongozi nilikuona Air Port, pale ulikuwa unafanya nini?
RIPOTA: Aah, kumbe uliniona? Mlivyojikausha nikadhani hamkuniona. Kuna mzigo wangu nilikuwa naufuatilia pale.
DIAMOND: Mzigo wapi? Naomba uniambie ukweli.
RIPOTA: Acha hizo dogo, unafikiri mimi nilikufuata wewe? Tena ningejua unafika leo, halafu ujio wenyewe ni huo, ningetega kamera zangu na tuwapige picha za kutosha.
DIAMOND: Aah, usifanye hivyo kiongozi.
Baada ya mazungumzo hayo, Diamond kila alipopigiwa simu hakupokea mpaka gazeti hili linanyanyuka kwenda kiwandani.
UFAFANUZI WA WEMA
Wema alipopigiwa simu na ripota wetu, alijibu kuwa yeye na Diamond hawajarudisha mapenzi, isipokuwa hivi sasa wako karibu kama marafiki wazuri kwa ajili ya kusaidiana mambo mbalimbali.
“Kusema ukweli kwa sasa sijafikiria kurejesha mapenzi na Diamond ila tupo karibu kama marafiki,” alisema Wema.
ZITTO NAYE
Jitihada za kumpata Zitto aweze kuzungumzia kurejea kwa penzi la Wema na Diamond kwenye tamasha aliloliandaa, hazikuzaa matunda. Muda wote naibu huyo wa Kambi ya Upinzania Bungeni, simu yake ilikuwa imezimwa.
WANANCHI WAMPONGEZA
Fununu kuwa Wema na Diamond wamerudiana zilivuma kwa kasi ndani ya mitandao ya kijamii na maoni ya wengi yakaelekeza pongezi kwa Zitto, kwani kabla ya hapo, mastaa hao walikuwa na uhasama mkubwa.
UNAKUMBUKA?
Malumbano yao kwenye vyombo vya habari? Diamond alipomfedhehesha Wema baada ya kukataa kupokea fedha zake alizomtuza kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam Machi mwaka huu? Je, kauli nzito za Mama Wema, Mariam Sepetu kwamba Diamond ni kijana mbaya na hafai?
JIULIZE SASA
Mpaka hapo bado unabisha kwamba mapenzi ni upofu? Unaendelea kukataa kwamba mapenzi hayaulizwi kwa nini? Diamond alipoachana Wema, alitua kwa Miss Tanzania namba mbili 2006-07, Jokate Mwegelo, je, penzi lao limeyeyuka au bado lipo kwa sura gani?
DENTI CHUO KIKUU ATEKWA AFARIKI DUNIA

MWANAFUNZI wa Chuo Kikuu Cha Usimamizi wa Fedha, (IFM) jijini Dar es Salaam, Agnes B. King’unza (pichani), amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kuokotwa akiwa hajitambui katika ufukwe wa Bahari ya Hindi jirani na Coco Beach.
Habari za kipolisi zinasema Agnes alitekwa kisha akaokotwa na msamaria mmoja ambaye kwa taarifa za awali anatajwa kuwa ni mlinzi wa nyumba moja maeneo ya Coco Beach, ambako ndiko alikokutwa akiwa hajitambui.
“Polisi na hata watu wengine wanahisi kuwa msichana huyo alitekwa kisha kutupwa na watu wasiofahamika, baada ya kufanyiwa ukatili wa kutisha kwa kunyweshwa kitu kinachodhaniwa kuwa ni sumu,” kilisema chanzo chetu cha habari ndani ya jeshi la polisi.
Habari zinasema baadaye mwanafunzi huyo ambaye alikuwa akichukua shahada ya mambo ya kodi, alipelekwa Kituo cha Polisi cha Oysterbay kisha askari hao wakamkimbiza Hospitali ya Agha Khan kwa matibabu.
Hata hivyo, habari zinasema madaktari wa Agha Khan baada ya kuona hali ya mgonjwa ilikuwa mbaya, walimpa rufaa na kumpeleka katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa uchunguzi na matibabu zaidi.
“Agnes alifariki jioni ya Julai 16, mwaka huu katika Hospitali ya Muhimbili na habari za kifo chake zilisababisha Chuo cha IFM kuzizima kwa wanafunzi kumlilia mwenzao,” kilisema chanzo hicho.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Charles Kenyela alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na akasema kwamba wasamaria wema walisema waliona Bajaj ikifika eneo alilotupwa Agnes wakadhani wanatupa mzigo.
“Walipokwenda kuangalia wakakuta ni mtu akiwa hoi hajitambui. Baada ya kupelekwa hospitali siku ya pili alikuja mama mdogo wa marehemu Agnes aitwaye Veronica Galus na akaleta taarifa kuwa binti yao huyo amefariki dunia. Polisi tunaendelea na uchunguzi kuwatafuta wahusika,” alisema Kenyela. Hata hivyo, kifo hicho kimeacha maswali mengi kuwa binti huyo alilishwa nini na nani?
Mzazi wa marehemu aliyetajwa kwa jina la Bernad King’unza mkazi wa Kimara Dar, hakupatikana kwa maelezo kwamba alikuwa safarini Iringa kwenye mazishi ya mpendwa wao huyo yaliyofanyika nyumbani kwao Kalenga, Iringa Julai 19, mwaka huu.

Tuesday, 19 June 2012

MSIMAMO WANGU WA SASA JUU YA KAULI YANGU "JOHN MNYIKA ATOA TAMKO"

Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika.
Nitatoa tamko la kina baadae kuhusu kilichotokea lakini kwa ufupi ubovu wa bajeti hii ni matokeo ya udhaifu wa Rais Kikwete, yeye ndiye aliyesaini Mpango wa Taifa wa miaka mitano kama Kiongozi Mkuu wa Nchi tena kwa wino mwekundu kama Amiri Jeshi Mkuu. Na yeye ndiye Mwenyekiti wa baraza la mawaziri, bajeti hii iliyoacha kuzingatia mpango wa Taifa imepita kwenye baraza alilloliongoza, pia kushindwa kutekelezwa kwa bajeti iliyopita ni matokeo pia ya udhaifu wa taasisi ya Urais.
Pia kwa mujibu wa Katiba Rais ndiye ambaye anapeleka bajeti bungeni, Waziri mwenye dhamana anapeleka tu kwa niaba. Rais amepewa mamlaka makubwa juu ya bajeti ibara ya 99 imeweka mipaka kuhusu mambo ambayo bunge lina mamlaka nayo huku ibara ya 90 inasema bunge likikataa bajeti rais…

KUMBE NYUMBA YA WEMA SIO YAKELISSA JENSEN KUSHINDA MISS REDD'S WORLD TANZANIA


Redd’s Miss World Tanzania, Lisa Jensen (katikati) akivishwa taji hilo na Miss Tanzania,Salha Israel katika hafla fupi iliyomalizika usiku huu kwenye kiota kipya cha maraha cha 327,Mikocheni jijini Dar es Salaam.kulia ni mshindi wa tatu kwenye kinyang’anyiro hicho,Pendo Laizer . Lisa amewashinda warembo wengine 9 katika shindano hilo dogo la kutafuta Mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Mwaka huu ya Miss World.

Mwakilishi wa Tanzania katika Mashindano ya Miss World 2012, Lisa Jensen akipunga mkono baada ya kushinda nafasi hiyo katika shindano dogo lililofanyika jana jijini Dar es Salaam na kushirikisha warembo 10 waliowahi kushiriki fainali za Miss Tanzania miaka ya nyuma. Lisa aliwashinda warembo wengine 9.

JACQULINE WOLPER AMENYANG'ANYWA GARI

Mwigizaji ‘five star’ kutoka tasnia ya filamu Bongo, Jacqueline Wolper Masawe, amenyang’anywa gari lake la kifahari aliokuwa akitanua nao katika mitaa mbalimbali ya jiji la Bongo.
Habari zenye ukweli 100% ambazo Teentz.com imezinyaka zinasomeka kuwa Wolper anayejulikana kama Amber Rose wa Bongo amenyang’anywa mkoko huo aina ya BMW X6 wenye thamani ya ‘ngawira’ za kibongo ML 170, sambamba na kupigwa ‘stop’ kukaribiana na mshefa aliyekuwa amemnunulia ndinga hiyo.
Kwa mujibu wa chanzo, hatua ya mshefa huyo kuamua kuchukua ndinga yake ni baada ya kugundua kuwa Wolper anatoka kimapenzi na ‘sharobaro’ mmoja anayemiliki duka maarufu la viwalo pande za Kinondoni.
Aidha chanzo hicho, kimeieleza Teentz.com kuwa hivi sasa mwanadada huyo ameamua kutembelea ndinga aina ya Noah aliyokuwa anaitumia hapo awali sambamba na kutoka kwa kuvizia kukwepa watu wake wa karibu washitukie mchongo.
Katika kuhakikisha kuwa ukweli unajulikana Teentz.com iliamua kumsaka na baada ya kupatikana Wolper aligeuka mbongo na kudai kuwa hakuna jambo kama hilo isipokuwa kilichotokea ni kuwa gari limepata matatizo na ameamua kulipeleka ‘garage’.
Alipotakiwa kueleza kuwa imekuwaje gari mpya kama ile aipeleke garage tene kwa siku tatu Wolper alisme hivi: “Bwana eeh wee jua liko ‘garage’ hayo maswali mengine mimi sitaki kuayasikia na kama una taka ugomvi endelea kuniuliza” alisema na kuondoka haraka eneo alilokuwa amekaa

Wednesday, 23 May 2012

STUDY ABROAD IN MALAYSIA

http://www.facebook.com/UCTISpotlight

DIDA AWAUZIA WAKE ZA WATU NYETI BANDIA

MTANGAZAJI wa Radio Times FM ambaye pia ni mjasiriamali, Hadija Shaibu ‘Dida’ anatajwa kuwauzia wake za watu nyeti bandia za kiume ambazo huzitumia kukata kiu zao.
Chanzo chetu ambacho ni mmoja wa wateja wa Dida kilichojitambulisha kwa jina la Mama Asuu wa Magomeni kimeliambia Ijumaa juzikati kuwa, yeye aliwahi kununua kifaa hicho kwenye duka la Dida lililopo Kinondoni jijini Dar.
“Mbona wanawake wengi wanajazana pale kununua kifaa hicho, niliwahi kumuuliza kama anavyo akaniambia nimpe fedha akienda China ataniletea, juzi ndiyo nikaenda kukichukua,” alisema mama huyo.
Katika kujua ukweli wa habari hizi mwandishi wetu alimtafuta Dida na alipopatikana alisema: “Huwa nikisafiri kwenda kuchukua mzigo China kuna wanawake huniagiza vifaa hivyo lakini kama ni suala la wanawake kujaa dukani kwangu wanafuata vingi.”

CHRISS BROWN ALIVYOCHANA KWENYE BILLBOARDS MUSIC AWARDS 2012


o it’s no secret that Chris can dance his a** off. Everyone knows it, and the boy don’t stop! So who cares if he doesn’t sing live sometimes, right? 
Apparently, a lot of people.
After receiving high praises from Brandy, who introduced his performance last night at the 2012Billboard Music Awards, Chris took to the stage for another high-energy performance of, ‘Turn Up The Music’. He tore up the stage for five straight minutes while surrounded by dancers, guys on bikes doing tricks and special stage lights. Although it was clearly about providing entertainment in the form of great choreography to Chris versus blowing the roof off of the building with his vocals, Chris’ critics definitely weren’t satisfied. Before he even had the chance to finish up his performance, a few celebs took to twitter to call him out for lip-synching:

Tuesday, 22 May 2012

Thanks to Jeremy Scott, Nicki Minaj’s Tour Fashion Rocks! (The Blonde Barb Pops and Locks in Pops of Color!)

D
The go-to designer of the moment, Jeremy Scott, lent his gifted designer hands to craft couture for Nicki Minaj’s Pink Friday tour this summer. In the colors of the season, neon pink and green, she kills the stage in Sydney, Australia, rocking ’90′s inspired looks with her dancers. Jeremy added street art charm with graffiti and gold spikes to her costume, but Nicki just wouldn’t be Nicki if she didn’t have a pair of tights on, would she? The dancers also wore graffiti’d bra tops with suspenders and neon biker shorts for an “I Heart the 90′s” moment.
Jeremy definitely gave the Pink Friday tour some high fashion style meets hip hop culture, and we can definitely appreciate it. Now let’s hope Jeremy can start styling Nicki for good! We kid…not really.

Disminders, is Nicki flying high and blazin’ in this ’90s inspired number?

Bongo Movies news: MADAI YA POLISI: MUME WA JACK PATRICK NI MUUZA UNGA

MUME wa msanii maarufu wa filamu nchini, Jack Patrick, Abdulhatif Fundikira anasakwa na polisi kwa madai kuwa anauza dawa za kulevya ‘unga’.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa Fundikira anasakwa baada ya mwanamke mmoja Mariam Mohamed Saidi,29, kudakwa na polisi wa Kitengo cha Kupambana na Kudhibiti Madawa ya Kulevya nchini ambapo amemtaja Fundikira kuwa ndiye mwenye dawa alizokamatwa nazo ambazo ilikuwa azisafirishe kuzipeleka Uturuki.
Uchunguzi wetu umebaini kuwa polisi walifika nyumbani kwa Fundikira saa 10 usiku wiki iliyopita lakini wakaambiwa kuwa hakuwepo, alikwenda kwenye msiba wa ndugu yake mikoani.
“Lakini hata mke wake hawakumkuta na hata walipopigiwa simu, zikawa hazipatikani na inavyoonesha wamepata fununu za kutafutwa na polisi hivyo kujikuta katika hali mbaya kila upende, wa dola na hata jamii,” kilisema chanzo chetu.
Gazeti hili lilimtafuta Kamanda wa Kikosi cha Kupambana na Kudhibiti Madawa ya Kulevya nchini, Godfrey Nzowa na kumuuliza kuhusu madai hayo naye alikiri kujua tukio hilo.
Akasema vigogo wa mtandao wa dawa za kulevya wamejulikana na kilichobakia ni kufuatilia nyendo zao na kuwadaka mmojammoja.
Akizungumza na mwandishi wetu wiki iliyopita ofisini kwake, Nzowa alisema kwamba orodha yao ni ndefu na kwamba Mei 16, mwaka huu kigogo mmoja akiwa na mke wake huko maeneo ya Buguruni Malapa wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam walitoroka kwao baada ya kupata taarifa kwamba mfanyakazi wao anayewasafirishia ‘unga’ nchi za nje,Mariam Mohamed Said ,29, amekamatwa.
Kamanda Nzowa amesema kwamba Mariam alikamatwa Mei 16, saa 9 usiku, Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere akiwa na kilo 10 za bangi zenye thamani ya shilingi milioni 12 zilizofichwa kwenye sanduku ambapo mtuhumiwa huyo amedai kwamba amekua akifanya biashara ya baibui.
“Uchunguzi unaonesha kuwa inawezekana isiwe ni biashara ya bangi tu bali hata aina nyingine ya dawa za kulevya wamekua wakisafirisha,” alisema.
Mariam alikamatwa akiwa na bangi mabunda 23 yaliyofungwa kitaalam wakati akijiandaa kupanda ndege ya kwenda Uturuki na alionyesha nyumba ya kifahari ambayo ina chombo maalum cha kunasa picha, CCVT.
Kamanda Nzowa alifafanua kwamba Mariam atafikishwa mahakamani wakati wowote upelelezi ukikamilika.
Hata hivyo, alikataa kutaja majina ya vigogo waliotoroka kwa madai kuwa ataharibu uchunguzi na amewaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi.

Amba Rose na Rapper Wiz Khalifa walivyo Toklezea kwenye Billboard Awards 2012

Video:Jordan Sparks & John Legend - Whitney Houston Tribute - Billoard Awards 2012

Jordan Sparks & John Legend - Whitney Houston Tribute - Billoard Awards 2012...As Seen On ©ABC...All Rights Reserved. i watched this that night and i started crying. whitney being such a great singer and all and you could see her daughter mouthing the words to this song you can tell there is so much love in this song from whitney. jordin did a great job and i think it was a great part of the show.