Subscribe:

Ads 468x60px

Tuesday, 22 May 2012

Bongo Movies news: MADAI YA POLISI: MUME WA JACK PATRICK NI MUUZA UNGA

MUME wa msanii maarufu wa filamu nchini, Jack Patrick, Abdulhatif Fundikira anasakwa na polisi kwa madai kuwa anauza dawa za kulevya ‘unga’.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa Fundikira anasakwa baada ya mwanamke mmoja Mariam Mohamed Saidi,29, kudakwa na polisi wa Kitengo cha Kupambana na Kudhibiti Madawa ya Kulevya nchini ambapo amemtaja Fundikira kuwa ndiye mwenye dawa alizokamatwa nazo ambazo ilikuwa azisafirishe kuzipeleka Uturuki.
Uchunguzi wetu umebaini kuwa polisi walifika nyumbani kwa Fundikira saa 10 usiku wiki iliyopita lakini wakaambiwa kuwa hakuwepo, alikwenda kwenye msiba wa ndugu yake mikoani.
“Lakini hata mke wake hawakumkuta na hata walipopigiwa simu, zikawa hazipatikani na inavyoonesha wamepata fununu za kutafutwa na polisi hivyo kujikuta katika hali mbaya kila upende, wa dola na hata jamii,” kilisema chanzo chetu.
Gazeti hili lilimtafuta Kamanda wa Kikosi cha Kupambana na Kudhibiti Madawa ya Kulevya nchini, Godfrey Nzowa na kumuuliza kuhusu madai hayo naye alikiri kujua tukio hilo.
Akasema vigogo wa mtandao wa dawa za kulevya wamejulikana na kilichobakia ni kufuatilia nyendo zao na kuwadaka mmojammoja.
Akizungumza na mwandishi wetu wiki iliyopita ofisini kwake, Nzowa alisema kwamba orodha yao ni ndefu na kwamba Mei 16, mwaka huu kigogo mmoja akiwa na mke wake huko maeneo ya Buguruni Malapa wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam walitoroka kwao baada ya kupata taarifa kwamba mfanyakazi wao anayewasafirishia ‘unga’ nchi za nje,Mariam Mohamed Said ,29, amekamatwa.
Kamanda Nzowa amesema kwamba Mariam alikamatwa Mei 16, saa 9 usiku, Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere akiwa na kilo 10 za bangi zenye thamani ya shilingi milioni 12 zilizofichwa kwenye sanduku ambapo mtuhumiwa huyo amedai kwamba amekua akifanya biashara ya baibui.
“Uchunguzi unaonesha kuwa inawezekana isiwe ni biashara ya bangi tu bali hata aina nyingine ya dawa za kulevya wamekua wakisafirisha,” alisema.
Mariam alikamatwa akiwa na bangi mabunda 23 yaliyofungwa kitaalam wakati akijiandaa kupanda ndege ya kwenda Uturuki na alionyesha nyumba ya kifahari ambayo ina chombo maalum cha kunasa picha, CCVT.
Kamanda Nzowa alifafanua kwamba Mariam atafikishwa mahakamani wakati wowote upelelezi ukikamilika.
Hata hivyo, alikataa kutaja majina ya vigogo waliotoroka kwa madai kuwa ataharibu uchunguzi na amewaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi.

1 comment: